Saturday, 24 December 2016
Chanjo ya Ebola yafanikiwa
Majaribio ya chanjo cha ugonjwa wa Ebola yamebainika kuwa yana uwezo zaidi dhidi ya virusi vya ugonjwa huo hatari.
Majaribio hayo yamefanyiwa nchini Guinea, mojawapo ya mataifa ya Afrika magharibi ambayo yalikumbwa na mlipuko wa ugonjwa huo, ambao ulimalizika mwaka huu.
Matokeo ya mwisho ya majaribio hayo, yaliyochapishwa kwenye jarida la maswala ya matibabu linalochapishwa nchini Uingereza, The Lancet, yanaonyesha kuwa takribani watu elfu sita waliopata chanjo hiyo, walionekana kuwa bila ugonjwa huyo siku kumi baadaye.
Miongoni mwa kundi lingine kama hilo, ambao hawakupewa chanjo, watu 23 walipatikana na virusi vya Ebola.
Mkurugenzi mkuu wa taasisi moja ya matibabu nchini Uingereza- Wellcome Trust, ameelezea matokeo hayo kama ya kufana mno.
Saturday, 17 December 2016
Friday, 16 December 2016
Virusi vya Zika vyagunduliwa nchini Tanzania.
Taasisi ya utafiti wa magonjwa ya binadamu, NIMR imethibitisha kugunduliwa kwa virusi vya Zika nchini Tanzania.
virusi hivyo vinaaminika kuchangia kuzaliwa kwa watoto wenye vichwa vidogo.Kuenea huku kwa kasi kwa virusi vya Zika ni kati ya magonjwa ya virusi yanayoenezwa na mbu.
virusi hivyo vinaaminika kuchangia kuzaliwa kwa watoto wenye vichwa vidogo.Kuenea huku kwa kasi kwa virusi vya Zika ni kati ya magonjwa ya virusi yanayoenezwa na mbu.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Taasisi hiyo, Dkt Mwele Malecela, virusi hivyo vimepatikana mkoani Morogoro, Mashariki mwa Tanzania na Mkoani Geita, kaskazini magharibi mwa Tanzania.
Utafiti huo ulifanyika kutokana na uhalisia kuwa kuna mazingira yanayowezesha kuzaliana kwa mbu wanaoeneza virusi hivyo
Thursday, 15 December 2016
Saturday, 12 November 2016
Maandamano kumpinga trump yaendeleaa
Katika miji kadhaa ya Marekani kwa usiku wa tatu mfululizo, Maandamano yameendelea nchini Marekani dhidi ya Donald Trump. Ikiwemo Mjini portland katika jimbo la Oregon polisi walitumia gesi ya kutoa machozi kuwatawanya mamia ya waandamanaji waliyokuwa wakiandamano kutoka kila upande wa barabara za mji huo,yakitarajiwa kuendelea katika jimbo la chicago baadaye leo.
Monday, 7 November 2016
TB JOSHUA atabiri mshindi uchaguzi Wa Marekani
Muhubiri maarufu Africa Tb Joshua Wa nchini Nigeria atabiri ushindi katika uchaguzi Wa marekani utakaofanyika Novemba 8 mwaka huu.
Ametabiri kwamba Bi. Hillary Clinton ataibuka na ushindi dhidi ya mpinzani wake Bwana Donarld Trump.
Katika ujumbe alioutuma kwenye ukurasa wake wa Facebook TB Joshua amesema kuwa Bi Clinton atashinda kwa ushindi mdogo, lakini atakabiliwa na changamoto nyingini - likiwemo jaribio la kupiga kwa kura ya kutokuwa na imani dhidi yake.

Subscribe to:
Posts (Atom)