Friday, 16 December 2016

Virusi vya Zika vyagunduliwa nchini Tanzania.

Taasisi ya utafiti wa magonjwa ya binadamu, NIMR imethibitisha kugunduliwa kwa virusi vya Zika nchini Tanzania.
virusi hivyo vinaaminika kuchangia kuzaliwa kwa watoto wenye vichwa vidogo.Kuenea huku kwa kasi kwa virusi vya Zika ni kati ya magonjwa  ya virusi yanayoenezwa na mbu.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Taasisi hiyo, Dkt Mwele Malecela, virusi hivyo vimepatikana mkoani Morogoro, Mashariki mwa Tanzania na Mkoani Geita, kaskazini magharibi mwa Tanzania.
Utafiti huo ulifanyika kutokana na uhalisia kuwa kuna mazingira yanayowezesha kuzaliana kwa mbu wanaoeneza virusi hivyo

No comments:

Post a Comment