Saturday, 24 December 2016
Chanjo ya Ebola yafanikiwa
Majaribio ya chanjo cha ugonjwa wa Ebola yamebainika kuwa yana uwezo zaidi dhidi ya virusi vya ugonjwa huo hatari.
Majaribio hayo yamefanyiwa nchini Guinea, mojawapo ya mataifa ya Afrika magharibi ambayo yalikumbwa na mlipuko wa ugonjwa huo, ambao ulimalizika mwaka huu.
Matokeo ya mwisho ya majaribio hayo, yaliyochapishwa kwenye jarida la maswala ya matibabu linalochapishwa nchini Uingereza, The Lancet, yanaonyesha kuwa takribani watu elfu sita waliopata chanjo hiyo, walionekana kuwa bila ugonjwa huyo siku kumi baadaye.
Miongoni mwa kundi lingine kama hilo, ambao hawakupewa chanjo, watu 23 walipatikana na virusi vya Ebola.
Mkurugenzi mkuu wa taasisi moja ya matibabu nchini Uingereza- Wellcome Trust, ameelezea matokeo hayo kama ya kufana mno.
Labels:
News
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment